Kichuya afunga baada ya mechi 9 - ALEX MWENDATZ

Breaking

Sunday, February 26, 2017

Kichuya afunga baada ya mechi 9



Kiungo Shiza Kichuya ameweka rekodi ya kuifunga Yanga mara mbili mfululizo.
Jana alifunga bao dakika ya 81, likiwa ni la pili na la ushindi kwa timu yake ya Simba.

Kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza ndiye aliyefunga bao la kusawazisha Oktoba Mosi mwaka jana, dakika ya  87 na kuzifanya timu hizo kwenda sare ya bao 1-1.
Kichuya pia amefunga goli la kwanza baada ya mechi tisa za ukame.
Shiza Kichuya akishangilia bao lake la ushindi dhidi ya Yanga leo
Mara ya mwisho kufunga goli ilikuwa ni Novemba 2 mwaka jana kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, alipofunga bao pekee dhidi ya Stand United kwa mkwaju wa penalti.
Kwa sasa amefikisha jumla ya magoli 10, nyuma ya Simon Msuva aliyefikisha magoli 11 na kuongoza msimamo wa wafungaji bora wa Ligi Kuu.

No comments:

Post a Comment