Na Baracka Mbolembole
Kushindwa kupandisha timu yoyote ligi kuu Tanzania bara msimu ujao kwa
Mkoa wa Dar es Salaam si pigo lakini ni dalili njema kwamba soka la
Tanzania linazidi ‘kutanuka’ kila pembe ya Tanzania. Lipuli FC
imerejea ligi kuu baada ya kusubiri kwa miaka takribani 15 na wamepanda
mbele ya timu za Friends Rangers na Mshikamano FC za Dar es Salaam.
Singida United nayo imerejea VPL baada ya kupita takribani miaka 16
ya Mkoa huo wa katikati mwa Tanzania kushindwa kuona michezo ya ligi na
huenda Njombe Mji FC ya Njombe ikaungana na timu hizo kongwe kupanda
ligi kuu msimu ujao kwa mara ya kwanza ikiwa itafanikiwa kupata walau
sare katika mchezo wao wa mwisho nyumbani vs Kurugenzi.
Licha ya kutokuwa na mdhamini Lipuli ilifanikiwa kutokana na juhudi,
umoja na mshikamano uliokuwepo miongoni mwa viongozi wa Chama cha soka,
uongozi wa klabu, serikali ya mkoa na wadau wote wa mpira ambao
walihakikisha timu hiyo inapata mahitaji muhimu.
Lipuli ilipangwa kundi A pamoja na Pamba FC ya Mwanza, African
Sports ya Tanga, Ashanti United, Friend Rangers, Polisi Dar FC,
Mshikamano FC ( zote za Dar es Salaam) na Kiluvya United ya Pwani.
Wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kwa sababu ni
kundi ambalo liliwafanya kusafiri mara nne kwenda Dar, mara moja Tanga
na mara moja Mkoa wa Pwani.
Kuongoza kundi ambalo lilikuwa na timu Nne kutoka Dar, moja Pwani na
nyingine ya Tanga si jambo rahisi kwa timu ambayo haikuwa na udhamini.
Lakini wamefanikiwa kupanda na kuziacha timu hizo ligi daraja la kwanza
huku Sports ikishuka hadi ligi daraja la pili.
Kundi hili awali lilionekana lingewapa nafasi nyingine mkoa wa Dar es
Salaam kuongeza timu katika ligi kuu lakini wameshindwa baada ya klabu
hizo kushindwa kutengeneza umoja katika klabu zao. Nakumbuka baada ya
kila timu kucheza michezo mitano niliandika mahala kuwa Lipuli, Polisi
Moro FC na Singida United zitapanda ligi kuu msimu ujao.
Maneno yangu yanaweza kutimia ikiwa Polisi Moro pia itafanikiwa
kupanda kutokakundi B japokuwa kiuhalisia nafasi hiyo ni ngumu baada ya
kuangusha pointi katika michezo miwili iliyopita. Nilisema hivyo baada
ya kuona hamasa iliyokuwepo kwa wanasoka wa mikoani ambao walidhamilia
na kuwekeza nguvu zao kuhakikisha timu zao zinapanda.
Kinondoni Municipal Council FC (KMC) ni timu pekee ya Dar es
Salaam ambayo ilijiandaa vizuri, licha ya kwamba ilipangwa kundi gumu
pamoja na timu za Mikoani timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni imekuwa na
mwenendo mzuri na watasubiri hadi siku ya mwisho kujua hatma yao.
Mji Njombe ambayo inaongoza kundi hilo la pili kwa alama Tatu zaidi
ya Polisi Moro na KMC ina nafasi kubwa zaidi ya kupanda na kunziacha
daraja la kwanza timu za JKT Mlale ya Ruvuma, Coastal Union ya Tanga,
KMC, Polisi Moro, Mbeya Warriors na Kurugenzi Iringa. Kumbuka tayari
timu ya Kimondo FC ya Mbeya imeshushwa daraja kutoka kundi hilo la pili.
Kundi C halikuwa na timu yoyote kutoka Dar es Salaam. Kundi hilo
lilikuwa na timu za Alliance School Academy ya Mwanza, JKT Mgambo ya
Tanga, Mvuvumwa FC ya Kigoma, Panone FC ya Kilimanjaro, Polisi Dodoma ya
Mpwapwa, Rhino Rangers ya Tabora na Singida United ambao wamepanda VPL
msimu ujao kutoka kundi hilo.
Kuanzia mwanzo hadi mwishoni mwa wiki iliyopita kundi hilo lilikuwa
na ushindani mkubwa baina ya timu tatu za Singida, Alliance na Rhino
huku timu ya Mvuvumwa ikishuka daraja.
KWANINI DAR ES SALAAM IMESHINDWA KUPANDISHA TIMU?
Rangers na KMC angalau zilikuwa na mwelekeo wa kupanda miongoni mwa
timu tano za Dar es Salaam ambazo lakini walishindwa dakika kutokana na
sababu za ndani na nje ya uwanja. KMC wamekwamishwa na uzoefu huku
Rangers wakianguka kwa kuamini kuwa timu yao ‘haipendwi na haitakiwi’ na
baadhi ya watawala wa soka la Tanzania.
Ashanti iliangushwa na hali ya uchumi, Mshikamano walijitahidi
kufanya vizuri lakini nao kama ilivyokuwa kwa KMC ilikwamishwa kwa
kiasi kikubwa na uzoefu. Polisi Dar haikujiandaa kwa lengo la kupanda.
Jambo zuri kwao ni kwamba hakuna timu ya Dar es Salaam iliyoteremka
daraja kwenda ligi daraja la pili hivyo wanaweza kujipanga upya kwa
ajili ya ligi daraja la kwanza msimu ujao.
Monday, February 13, 2017
New
TIMU 5 KUTOKA DAR LIGI DARAJA LA KWANZA
About SPORTS ROOM
SoraTemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of SoraTemplates is to provide the best quality blogger templates.
MICHEZO
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment