Kabla ya mchezo wa Jumamosi dhidi ya Tottenham, Liverpool haikuwa
imeata ushindi kwenye michezo ya ligi kuu ya Uingereza tangu mwaka 2017
uanze. Hii ilipelekea kuwapo kwa hisia tofauti na mtoto mmoja wa
aliyekua mchezaji wa Rugby wa Afrika Kusini, Joost van der Westhuizen
aliamua kuandika barua iliyogusa hisia za wengi akimwomba baba yake
“tafadhali mwambie mwenyezi Mungu mbinguni kuwa Liverpool inatakiwa
kushinda.”
Mchezaji nguli huyo wa zamani wa timu ya Rugby ya Afrika Kusini
maarufu kama Springboks alikutwa na matatizo ya nuroni tangu mwaka 2011
na alikutwa na mauti mapema mwezi huu, tarehe 6 mwezi Februari.
Na mtoto wa Van der Westhuizen anayeitwa Jordan, aliandika barua kwa
baba yake, akimwomba aifikishe kwa mwenyezi Mungu kabla Liverpool
haijakutana na Tottenham.
Barua ilisambaa kuitia mtandao wa Twitter, baada ya golikipa wa
zamani wa Liverpool, Sander Westerveld, kuweka bandiko kwenye ukurasa
wake wa mtandao huo akisema “Liverpool imeshinda, hakuna cha ajabu na
asante kwa kumwomba baba yako, Jordan!
Kisha akamalizia na “RIP Joost van der Westhuizen”.
Kwenye barua hiyo, Jordan anaandika: “Ahsante baba kwa kila kitu lakini kubwa ya yote kuwa bora kwa namna unayoweza!’
“We ni mchezaji bora wa Rugby duniani na mie nataka kuwa mwanamichezo
bora kama wewe kwa sababu ulisema natakiwa kupambana na kufanya
juhudi.”
“Nitakupenda siku zote, iwe mwezini au duniani. Baba tafadhali naomba umwambie Mungu kuwa Liverpool inatakiwa kushinda.”
“Nakupenda sana, Jordan xxx”
Van der Westhuizen, ambaye aliichezea Springboks michezo 89, aliagwa kwenye heshima siku ya Ijumaa huko Pretoria.
Monday, February 13, 2017
New
MTOTO NUKSI ONGEA NA MUNGU BABA LIVER POOL ISHINDE
About SPORTS ROOM
SoraTemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of SoraTemplates is to provide the best quality blogger templates.
MICHEZO
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment