Mwamuzi kutoka Uingereza Mark Clattenburg ambaye hivi karibuni
alitangazwa kuwa mwamuzi bora zaidi duniani, alichezesha mchezo wa ligi
kuu nchini Uingereza siku ya Jumamosi, February 11 kati ya Arsenal na
Hull city aliwaomba msamaha wachezaji wa Hull City kwa kulikubali goli la Sanchez alilofunga kwa mkono katika dk 34 ya mchezo.
Mchezaji wa Hull city Andrew Robertson amesema kuwa baada ya
kumalizika kwa kipindi cha kwanza mwamuzi huyo wa kati aliwafata na
kuomba msamaha kwa kosa hilo,.
“Tulipokuwa tunatoka mapumziko, mwamuzi alituomba msamaha na akasema
mpira ulishikwa , kwa hiyo lazima atakuwa aliangalia tena kipindi cha
mapumziko na akaona kuwa alikosea.
Ilitokea kwa haraka sana, ni vigumu mno kwa mwamuzi, lazima ujisikie hali ya huruma kwake ” Robertson aliiambia Sky Sports 1.
Katika mchezo huo Arsenal waliibuka na ushindi wa mabao mawili kwa
sifuri ,magoli yote yalifungwa na Alexis Sanchez dakika ya 34 Pamoja na
dakika ya 90’+3′ kwa mkwaju wa penati.
Monday, February 13, 2017
New
Mwamuzi Mark Clattenburg awaomba msamaha klabu ya Hull City
About SPORTS ROOM
SoraTemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of SoraTemplates is to provide the best quality blogger templates.
MICHEZO
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment