New
Kutokana na mwenendo wa Leicester City kuendelea kuwa mbaya, beki
wa zamani wa Arsenal, Martin Keown amedai kuwa kiungo mshambuliaji wa
Leicester City, Riyad Mahrez ameshindwa kung’ara hivi karibuni kutokana
na kuonyesha tabia za uvivu.
 |
Riyad Mahrez |
Akizungumza
kama mchambuzi wa soka kwenye runinga Keown alisema anaamini Leicester
imeshindwa kuwika msimu huu kama ilivyokuwa msimu uliopita kutokana na
wachezaji wa timu hiyo kutoonyesha bidii.
Mahrez alikuwemo
katika kikosi kilichofungwa 2-0 na Swansea, jana huku akishindwa
kuonyesha ubora kama ilivyokuwa msimu uliopita na kuifanya timu hiyo
sasa kuwa hatarini kushuka daraja.
 |
Martin Keown |
“Alikuwa
na uwezo wa kuwasumbua wapinzani anavyotaka, hilo sasa halifanyiki kwa
kuwa kuna uvivu fulani na haonyeshi kama anataka hilo litokee,” alisema
Keown.
No comments:
Post a Comment