TUTALINDA HESHIMU BURUNDI KATIKA MCHEZO WA MARUDIANO - ALEX MWENDATZ

Breaking

Monday, February 13, 2017

TUTALINDA HESHIMU BURUNDI KATIKA MCHEZO WA MARUDIANO

Mchezaji wa KVZ Sultan Juma ambae alifunga bao la pili na la ushindi katika mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika KVZ walipoifunga Messenger Ngozi kutoka Burundi mabao 2-1 mchezo uliochezwa jana katika uwanja wa Amaan amesema katika mchezo wa marejeano watapigana kuliko walivyopigana katika mchezo wa jana.


“Leo (Jana) tumepigana na tunashukuru kupata alama 3 nyumbani, sasa katika mchezo wa pili huko kwao tutapigana kuliko huku ili tulinde heshma ya Zanzibar,” alisema Sultan.

Nae Ubasenga Danny ambae ni captain wa Messenger Ngozi amekiri wana kazi kubwa katika mchezo wa marejeano ambapo amesema KVZ si wabaya kama walivyotegemea.


“Sasa akili yetu yote ni kupindua matokeo haya tulofungwa lakini tunajua kuwa tuna kazi pevu sana huko nyumbani, ila sina wasi wasi sana kwa vile ukicheza nyumbani unapata faida fulani, tutawafunga lakini ni mechi ngumu sana,” alisema Danny.

Wababe hao watarejeana Jumamosi ijayo ya Februari 18, huko mjini Bunjumbura Burundi nyumbani kwa Messenger Ngozi.

No comments:

Post a Comment